Mirabaha ya Wasanii Gizani

SERIKALI ilisema itaanza kulipa mirahaba ya kazi za wasanii kuanzia Desemba mwaka huu kupitia makusanyo yatakayopatikana kwenye vyombo vya habari vitakavyotumia kazi zao lakini hadi sasa siku tatu zimesalia mwaka ukatike na mambo ni ZZZZZ, yaani giza nene.

 

Ubashiri wa wengi ulionesha kuwa, huwenda jambo hili likashindikana kutokana na wasanii wenyewe kugawanyika kwa baadhi kukubali kulipwa na wengine kugoma.

 

Wasanii hasa chipukizi walipinga makusanyo hayo kwa kusema mpango huo utakuja kuua sanaa ya Bongo kwa sababu vyombo vingi vya habari vitasita kutumia kazi za wasanii kwa kuogopa malipo.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii