Staa wa muziki Bongo Alikiba amemjibu Maua Sama kwa kumwambia hakuna mtu wa kumpiga akirudia kusikiliza wimbo wake wa Zai, Utu ya Alikiba na I wish ya Kusah.
Kupitia ukarasa wa Twitter Maua Sama ameandika kwamba “Kwani ikitokea hujaimba Amapiano unaweza kufutiwa cheti cha usajili BASATA au utapokonywa NIDA & Passport?”
“Nipo zangu sehemu hapa nakunywa soda nasikiliza Zai, Utu & I wish (On Repeat) nipo Airport njooni mnipige”
Alikiba akacomment kwenye tweet hiyo kwa kuandika “Hakuna wa kukupiga Zai wangu”.