VIAN MUSIC ANAKIRI KUWA MZIKI WA UGANDA NI CHANGAMOTO.

Baada ya kufanikiwa kupokelewa vizuri na mashabiki kutoka nchini uganda miaka miwili iliyopita kupitia wimbo wake uitwao kili wakati akiwa ameshirikiana na gravity ommutuju kutoka uganda.

 

Vian music ni moja ya msanii ambaye anachipukia kutoka nchini uganda ambaye hivi karibuni ameonyesha kuwa ukiwa na nia jambo lolote linawezekana kwa kufanya kolabo na msanii pallaso ambaye ni mdogo wake na mwanamuziki jose chamelione wimbo uitwao omu.

Vian music amefanya mahojiano kupitia kipindi cha kikwetu ndani ya jembe fm mwanza na kuzungumza mambo mbali mbali kuhusu sanaa ya muziki nchini uganda.

 

Vian Aliulizwa Kuhusiana Na Changamoto Kuu Ambayo Anakumbana Nayo Akiwa Kama Msanii Nchini Uganda Na Kujibu Hivi:-

 

“Sio Rahisi Kuwa Msanii Nchini Uganda Changamoto Kubwa Tuliyonayo Ni Gharama Kubwa Ya Kwenda Studio Kurekodi Lakini Pia Gharama Ya Kufanya Video Yenye Ubora Na Hata Kukosa Muda Wa Kulala Ni Changamoto Sana “

Alisema Vian Ambaye Pia Anatizamia Kufanya Kazi Na Wasanii Wengi Zaidi Pindi Atakapo Pata Nafasi Hiyo Ndani Ya Uganda Nan Je Ya Uganda.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii