Msanii wa muziki wa miondoko ya hiphop na afro beat zara ozay mwenye asili ya nchini nigeria ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa beau_e akiwa ameshirikiana na shun breezy kutoka huko huko nchini Nigeria.
Zara ozay ambaye ana kiu ya kufanya kazi na wasanii mbali mbali kutoka afrika ya mashariki akifanya mahojiano kupitia kipindi cha burudani cha hitzone ndani ya jembe fm aliulizwa anapenda nini kuhusu muziki wa tanzania na ni msanii gani angetamani kufanya nae kazi na alijibu:-
“napenda sana uandishi na melodi ya muziki wa tanzania kwani muziki una ladha ya tofauti na yenye kuvutia sana na wasanii ambao natamani kufanya nao kazi kutoka tanzania na harmonize na diamond platnumz wanaimba vizuri sana na naupenda sana muziki wao”
Alisema zara ozay ambaye aliongeza kuwa kwa sasa yuko mbioni kufanya ziaza yake ya muziki afrika ya mashariki .