Jaguar Arejelea Muziki baada ya Kushindwa Kutetea Kiti Chake, Atoa Kibao Kipya.

Mwanamuziki Charles Njaguar Kanyi almaarufu Jaguar ametoa wimbo mpya wa kuvutia na mwimbaji wa Uganda, Ambassada.

Baada ya uteuzi uliokuwa na upinzani mkali, mbunge huyo wa zamani wa Starehe alipoteza uteuzi wa UDA kwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Simon Mbugua.

Jaguar alitangaza kuwa ameanza tena kuvuma huku akizindua wimbo wake mpya na mwimbaji wa Uganda kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wimbo huo unaoonekana unaanza huku mwanasiasa huyo wa zamani akigonga kengele kwenye viwanja vya kanisa na kumwomba Mungu amtumie kama chombo cha kueneza wema.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii