Mume wa Nick Minaj Ahukumiwa Kifungo cha Nje Mwaka Mmoja na Faini

mume wa rappa Nicki Minaj, Kenneth Petty (44) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu chini ya uangalizi wa mahakama pamoja na kifungo cha nyumbani mwaka mmoja.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya Petty kukiri kushindwa kujisajili kama mkosaji kingono (Sex Offender) baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana wa miaka 16 mwaka 1995, ambapo mwaka 2020 alihitajika kujisajili kama mkosaji wa kingono.

Aidha, mahakama imemtaka alipe faini ya $55,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 128 za Kitanzania Nicki na Petty ambao kwasasa wanaishi huko California, mwaka 2020 walibahatika kupata mtoto wao wa kwanza wa kiume.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii