Mwanamuziki Jennifer Lopez ‘J Lo’ Afunga Ndoa Tena na Staa wa Filamu Ben Affleck

Jennifer Lopez almaarufu JLO; ni staa wa filamu na muziki wa Hollywood nchini Marekani ambaye yeye na mchumba wake, Ben Affleck wamefunga ndoa huko Las Vegas.

JLO amethibitisha “Tulifanya hivyo. Mapenzi ni jambo zuri Upendo una ukarimu na inageuka kuwa mapenzi yana uvumulivu. Uvumilivu wa miaka ishirini Harusi hiyo inakuja miaka 17 baada ya kusitisha uchumba wao wa kwanza.

Habari za wanandoa hao kurudi pamoja mwaka jana ziliwafanya mashabiki wawe na msisimko huku wakionesha hadharani mapenzi yao yaliyofufuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Wawili hao walikutana kwenye maandalizi ya Sinema ya Gigli mwaka 2002 na wakachumbiana mwaka 2003, lakini walivunja uchumba wao mwaka uliofuata wakilalamika kufuatiliwa sana na vyombo vya habari.

Hata hivyo, tangu warudiane, mara kwa mara wamekuwa wakiachia picha na video mtandaoni za likizo na matukio ya kimapenzi wakiwa na familia zao na kuwafanya mashabiki kuwaita wanandoa hao jina la Bennifer.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii