Paula Kajala au Pau; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) nchini Tanzania ambaye aliapa kwamba labda afe ndipo mama yake, Kajala Masanja amrudie ex-wake, Harmonize, lakini sasa kibao kimegeuka.
Nyuma ya pazia, stori za ndani zinasema kuwa, baada ya Harmonize au
Konde Boy Mjeshi ambaye ni msanii wa Bongo Fleva kuona Paula anaendelea
na msimamo huo kwa mama yake ambaye ameshakubali kumrudia na maisha ni
bambam, jamaa huyo ameamua kutumia ‘plan B’.
Harmonize au Harmo anadaiwa kumwagia Paula mamilioni ya pesa ili
kumlainisha; na kama wasemavyo, hakuna uchawi mkubwa zaidi ya pesa hivyo
amefanikiwa kwa sababu mrembo huyo tayari ameungana na mama yake
nyumbani kwa jamaa huyo, Salasala jijini Dar na anamsalimia ‘Shikamoo
Daddy’.
Paula muda siyo mrefu atazindua bonge la duka la nguo jijini Dar ambapo tayari fremu ya shilingi milioni nane imelipiwa na mtaji wa shilingi milioni 14 umetolewa na Harmonize.
Mtu wa karibu wa Paula amedokeza kuwa, kwa sasa Paula anapiga picha
matata za mavazi za tangazo la duka hilo ambapo litaibua mjadala kwamba
ni lake au siyo lake anafanya tu matangazo ili liendelee kuwa gumzo.
Inaelezwa kuwa, Harmonize kwa sasa anawamwagia pesa mama na mwanawe
kwani haamini kama msamaha wake ungekubalika huku wawili hao wakiendelea
kushambuliwa kwa kukubali msamaha huo.
Mwijaku; ni mtangazaji na muigizaji maarufu Bongo ambaye ni mtu wa
karibu wa Harmonize akienda nyumbani kwake muda wowote ambaye
anathibitisha Paula kukubali kumfuata nyumbani kwa jamaa huyo na
wanainjoi maisha kwani kwa sasa mambo yapo sawa kabisa; wamesahau
yaliyopita na sasa wanaganga yajayo