DIAMOND AMPONGEZA HAJI MANARA

Msanii wa bongo fleva  Nassibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amempongeza Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara, kufuatia Klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa 28 wa Tanzania Bara jana Jumatano (Juni 15).


Young Africans ilijihakikishia kuwa Bingwa wa Tanzania Bara, baada ya kunyakua alama tatu za mchezo wake na Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Diamond amempongeza Manara ambaye alijiunga na Young Africans mwanzoni mwa msimu huu 2021/22 akitokea Simba SC, kwa sababu zilizotajwa kutokua na maelewano mazuri na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Katika Ujumbe wa Diamond amethibitisha kufahamu madhila aliyopitia Haji Manara kabla ya kuondoka Simba SC, huku akiandika Mungu wetu ni mkubwa kuliko fitna za binadamu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii