Jana June 30 kulikuwa na taarifa zinasambaa mitandaoni kuhusu ujio wa Msanii wa Nigeria, Kizz Daniel kutumbuiza nchini Tanzania.
Lengo la Str8upvibes na Big Step Consultancy kuwapa mashabiki wetu kile wanachotaka hususani kwenye masuala ya matamasha hivyo mwaka huu kuna vingi nimepanga kufanya mimi na timu yangu, hivyo taarifa zilizoenea kuhusu Kizz daniel ni kweli na mazungumzo ya awali yalifanyika pamoja na Steve kutoka Big Step baada ya kukutana nae Dubai’- Sniper Mantana
“Na katika mazungumzo yetu alikuwa na hamu kubwa ya kurudi tena Dar es Salaam kwani mara ya mwisho sisi ndio tulimleta Mwaka 2016, hivyo Mashabiki na wadau wa burudani waliopo Dar wakae karibu na mitandao yetu ya kijamii Str8upvibes na Big Step Consultancy tutataja tarehe husika lini atatua Dar na wapi ambapo burudani hiyo itatolewa”– Sniper Mantana
‘Kingine kwamba tunaenda na mabadiliko ya kigiditali tumebadilika unajua hapo awali mashabiki wetu walikuwa wanapata shida katika masuala ya ununuzi wa tiketi hivyo tumelitatua ambapo tiketi zitakuwa zinapatikana katika application ya Big Step Consultancy hivyo muda wowote tutaanza kutangaza mchakato mzima’- Sniper Mantana