Kauli ya Ben Pol

MWANAMUZIKI wa Bongo Flava Ben Pol, hatamani tena ndoa kwa sasa baada ya mahusiano yake na binti Mkenya Anerlisa Muigai kuvunjika.

Akipiga stori na safu hii hivi majuzi kwenye ziara yake Nairobi, anakiri kuwa japo bado ana imani kwenye ndoa, kwa sasa hatamani.

“Sijakata tamaa kwenye ndoa. Itafika wakati nitaoa tena ila sio kwa sasa. Sasa hivi sihisi hivyo. Sina mvuto wala matamanio ya kuwa kwenye ndoa tena. Itanichukua muda kuwa tayari tena,” kafunguka.

Ndoa yake na Anerlisa iliingia mdudu baada ya mwaka mmoja tu na kumpelekea jamaa kuwasilisha ombi la talaka Aprili 2021.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii