FAT JOE JAMBO NILILOWAHI KUHOFIA MAISHANI NI KUWA BABA NIKIWA NA MIAKA 19

Msanii Wa Muziki Wa Hip Hop Kutoka Nchini Marekani Rapa Fat Joe Ambaye Huwezi Kumzungumzia Bila Kuitaja Ngoma Ya Lean Back Na Nyingine Nyingine.

Kila June 19 Ni Siku Ya Kumbukumbu Yasiku Ya Baba Duniani Na Hivyo Imekuwa Ikisherehekewa Kwa Namna Mbali Mbali Huku Watoto Wakionyesha Mapenzi Kwa Baba Zao N Ahata Wababa Kuonyesha Mapenzi Kwa Watoto Wao.

 

Sasa Siku Ya Jana Ilikuwa Siku Hiyo Ambayo Wengi Waliandika Vingi Kuhusu Baba Zao Walio Hai N Ahata Waliotangulia Mbele Ya Haki.

Sasa Rapa Fat Joe Aliamua Kuweka Wazi Namna Ambavyo Haikuwa Rahisi Kwa Upande Wake Kuwa Baba Akiwa Na Umri Wa Miaka 19.

 

Rapa Fat Joe Aliketi Na Hiphopdx Kujadili Kuwa Mzazi Kwa Watoto Wake Watatu. Rapa Huyo Wa New York Ni Baba Wa Ryan Cartagena, Joey Cartagena, Na Azariah Cartagena.

Amenukuliwa Akisema Kuwa;_

 

"Huo Ulikuwa Wakati Wa Kutisha Zaidi Maishani Mwangu,Likuwa Inatisha. Mimi Mwenyewe Nilikuwa Mtoto Tu. Nilikuwa Tu Nimepata Dili Langu La Rekodi. Sikuwa Na Wimbo Hata Nje. Ilikuwa Kweli, Ya Kutisha Sana Kuwa Mchanga Sana Na Kuwa Na Jukumu Kubwa, Kwa Hivyo Hilo Lilikuwa Jibu Langu La Kwanza.

Alisema Fat Joe Ambaye Mpaka Sasa Anajivunia Watoto Wake Wote Na Anafuraha Kuwa Baba Yao Na Kuwa Sehemu Ya Maisha Yao Hapa Duniani Lakini Kama Mtu Yeyote Angemuuliza Kuhusu Kuwa Baba Kwa Mara Ya Kwanza Kwake Haikuwa Jambo Zuri Kama Ambavyo Wengine Hufurahia Jambo Hilo.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii