MISS CHANTY :AVUNJA UKIMYA NIMEKUWA NIKITESWA MARA NYINGI NA MPENZI WANGU.

Miss chanty ni moja kati ya mwanadada ambaye alipata umaarufu kwa kuwa kwenye mahusiano na mchekeshaji kutoka nchini Kenya eric omondi ambaye walidumu kwenye mahusiano kwa miaka kadhaa na baadae kuamua kuachana kutokana na sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wao.

 

Huku ikifahamika Zaidi kuwa miss chanty ni raia wa Italy ambaye pia anaasili ya Kenya.

Miss chanty baada ya kuachana na eric omondi aliamua kuingia kwenye mahusiano na mwanaume ambaye anafahamika kwa jina la Nicola ambaye tangu alipoingia katika mahusiano na mwanaume huyo chanty hakuwa mtu wa mitandao sana kama ilivyokuwa zamani.

Sasa siku kadhaa zilizopita kuna tukio ambalo limemkuta mwanadada huyo kwa kupigwa na mpezni wake huyo ambaye alimvamia katika nyumba anayoishi na kumjeruhi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram miss chanty ameandika ujumbe 

 

Ameandika Miss Chanty kuwa Mpenzi wake huyo amekuwa akimtesa sio mara moja wala mara ya kwanza ni mara nyingi lakini siku zote Jamaa huyo amekuwa akimkataza kutumia na hata kumuonya kusema lolote mtandaoni tena kwa kumtishia Maisha Yake.

lakini pia Chanty ameeleza amesikitishwa na kitengo cha GBV huko kenya kwa jinsi kilivyo shindwa kulipa umakini jambo lake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii