AKOTHEE:HABARI ZA MAHUSIANO KUVUNJIKA SASA BASI

Msanii wa muziki kutoka nchini kenya pamoja na mfanyabiashara kutoka nchini humo esther akoth kokeyo maarufu kwa jina la akothee wikiendi iliyopita alifanikiwa kuzindua kitabu chake ambacho kinaitwa “akothee quotes” pamoja na kuzindua e p yake ambayo ameipa jina la “akothee the lioness” yenye nyimbo 8 ndani yake huku nyimbo mbili akiwa ameshirikiana na tony nyadundo pamoja na kamanu.

Sasa wengi walifahamu akothee ambaye ni mama wa watoto watano alikuwa katika mahusiano na bwana ambaye alikuwa ni meneja wake pia aitwaye nelson lakini chakushangaza katika uzinduzi wa matukio hayo muhimu bwana huyo hakuonekana.


Sasa kupitia ukurasa wake wa instagram akothee amebainisha wazi kuwa sasa yupo single na ameamua kuweka nguvu zake katika kuitangaza ep yake pamoja na kitabu chake kwani mambo ya kuvunjika kwa mahusino yanatosha kwa sasa.

 

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii