Caitlyn Jenner Ambaye Zamani Alifahamika Kwa Jina La Bruce Jenner Baba Mzazi Wa Kim Kardashian Ambaye Aliamua Kubadili Jinsia Na Kuwa Mwanamke.
Caityln Ameibuka Mara Baada Ya Kim Kardashian Kuchana Na Kanye West Na Kuamua Kuendelea Na Maisha Yake Huku Akiwa Katika Mahaba Mazito Na Pete Davidson Ambaye Ni Moja Ya Mwanaume Ambaye Familia Ya Kardashian Imekuwa Ikimzungumzia Vizuri Sana Huku Kim Akijinadi Kuwa Mtu Mwenye Furaha Zaidi Katika Mahusiano Yake Ya Sasa.
Caitlyn Jenner Akifanya Mahojiano Na Chanzo Cha Habari Cha Entertainment Tonight Ameweka Wazi Jinsi Ambavyo Anafikiri Binti Yake Alikuwa Anakutana Mahusiano Ambayo Ni Magumu Na Hayana Furaha.
“Mimi Sina Tatizo Na Kanye West Lakini Naweza Kusema Mwanangu Kimberly Amekuwa Katika Mahusiano Tofauti Tofauti Na Hayakuwa Mazuri Lakini Mahusiano Ambayo Yalikuwa Mabaya Zaidi Kwa Mwanangu Ni Mahusiano Yake Na Kanyewest.”
Alisema Caityln Ambaye Anaamini Kim Hakuwa Mwenye Furaha Katika Ndoa Yake Na Kanye.