ZARI THE BOSSLADY :MSIMU WA PILI WA “YOUNG RICH AND FAMOUS “ UNAKUJA

Zarinah Hassan Maarufu Kwa Jina La Zari The Bosslady Ambaye Ni Raia Wa Uganda Mwenye Makazi Yake Huko Afrika Ya Kusini.

 

Zari Ambaye Ni Mama Wa Watoto Watano Watatu Akiwa Amepata Na Marehemu Mumewe Ivan Ssemwanga Na Wawili Akiwa Amepata Na Msanii Maarufu Kutoka Tanzania Diamond Platnumz .

Licha Ya Umaarufu Wa Zari The Bosslady Ni Moja Ya Wanawake Waliofanikiwa Katika Nyanja Tofauti Tofauti Jambo Ambalo Linafanya Baadhi Ya Mabinti Kuvutiwa Na Aina Ya Maisha Anayoishi Mwanamama Huyo.

Ikiwa Ni Miezi Kadhaa Tangu Kutoka Kwa Tamthiliya Ya “Young Rich And Famous” Ambayo Imehusisha Watu Mbali Mbali Maarufu Kutoka Africa Nzima Ikiwemo Nigeria ,Tanzania ,Uganda ,Afrika Ya Kusini N.K



Ni Tamthiliya Ambayo Iliachiwa Kupitia Mtandao Wa Netflix Ambayo Pia Ilifanikiwa Kupata Watazamaji Wengi Kwani Ilikuwa Na Maudhui Tofauti Tofauti Kuhusu Maisha Ya Kila Siku Ya Watu Maarufu Na Jinsi Ambavyo Wanapitia Changamoto Na Namna Wanavyoweza Kuzitatua Kama Binadamu.

Zari Ambaye Ametembelea Nchini Kenya Mapema Leo Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Katika Uwanja Wa Ndege Wa Jomo Kenyatta Ameweka Wazi Kuhusu Tamthiliya Hiyo Na Kusema Haya.

“Ilikuwa Ni Ujuzi Mzuri Kushiriki Katika Tamthiliya Hiyo Ambayo Pia Ndani Ya Muda Mchache Ilifanikiwa Kuwafikia Watu Wengi Zaidi Lakini Siwezi Kusema Sana Kuhusu Msimu Wa Pili Nani Atakuwepo Ndani Ya Msimu Wa Pili Lakini Msimu Wa Pili Unafata Hivi Karibuni.”

Amesema Zari Ambaye Amewasili Nchini Kenya Kwaajili Ya Shughuli Ya Uzinduzi Wa Nyumba Ya Kifahari Ya Moja Ya Moja Ya Watengenezaji Wa Maudhui Ya Mtandaoni Maarufu Wajesus Family.

 

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii