JESSIE J NILIPOTEA KWENYE MUZIKI BAADA YA BABU YANGU KUFARIKI

Jessica Ellen Cornish Maarufu kama Jessie J ni moja ya Msanii kutoka nchini marekani ambaye aliwahi kufanya vizuri sana na moja ya ngoma ambayo ilimtambulisha vizuri na wengi kumfahamu ilikuwa ni ngoma ambayo ilifahamika kwa jina la Price Tag.

Jessie J alipotea katika ulimwengu wa Muziki jambo embalo mashabiki zake wengi walihoji ni papi hasa Msanii huyo amejiweka au kujificha lakini Jessie J ameeleza kilichofanya yeye apotee katika ulimwengu wa Muziki katika mahojiano aliyoyafanya siku za hivi karibuni.


Kupitia mahojiano aliyoyafanya na hanzo cha habari cha A Diary of a CEO Jessie J amezungumza Mengi kuhusu masha Yake binafsi na hata masha Yake ya Muziki na jinsi alivyopambana kuweza kurejea tena licha ya maumivu ,Machozi ambayo aliyapitia katika safari Yake.

Lakini swali la wengi lilikuwa ni kwanini alipotea katika muziki na Jessie J alijibu kwa ifuatavyo:-

"Nilipotea katika Muziki baada ya kuondokewa na babu yangı kipenzi ambaye nilikuwa nampenda sana na alikuwa kama mwalimu wangu katika Muziki kwani alikuwa akifanya pia sanaa hivyo ni mambo Mengi alinisadia katika Muziki ambayo nilikuwa siyajui,kwahiyo alipofariki ilikuwa wakati mgumu sana kwangu jambo ambalo niliona bora nikae pembeni niache Muziki kwanza ili kurudi kuwa sawa na ikanilazimu niende kuvunja mkataba na lebo iliyokuwa inanisimiamia na hata kufuta miziki ambayo nilikuwa nimeandika na kurekodi yani sikutamani hata nyimbo zangu mwenyewe mwaka 2016."

amezungumza Jessie J ambaye anakiri pia ilikuwa wakati ambayo alihitaji kupata timu ya watu ambao wataenjoy na kufurahi pamoja lakini watambue thamani yake kwao na kwake.




Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii