Msanii wa Bongo Fleva Gigy Money Aliamsha Tena

MOURAD Alpha almaarufu Mo J; ni mtangazaji wa Radio Clouds FM ambaye dunia inajua ni baba mzazi na halisi wa mtoto Mayra aliyezaa na msanii wa Bongo Fleva, Gigy Money.

Mo J na Gigy walikutana miaka kadhaa iliyopita katika Kituo cha Redio cha Choice FM; wote wakiwa watangazaji kisha walianzisha uhusiano wa kimapenzi.

Wakati huo, Mo J na Gigy walikuwa wakitangaza kipindi kimoja cha malavidavi.

Uhusiano wao ulikwenda mbali zaidi baada ya Mo J kumpa mimba Gigy na hatimaye akajifungua mtoto ambaye ni Mayra.

Baada ya kupata mtoto, watu hawa hawakudumu kwenye uhusiano, kila mmoja akaelekea anapopajua

Gigy akapita huku na huku na hatimaye sasa ametulia kwa jamaa aitwaye Crey.

Kwa upande wake, Mo J naye hivi karibuni alifunga pingu za maisha na mwanamke wake mwingine.

Gigy siku zote amekuwa akimpa makavu Mo J katika mahojiano mbalimbali akidai kuwa jamaa huyo hamtunzi au amemtelekeza mwanawe huyo hivyo anapambana peke yake kumlea mtoto huyo ilihali baba yake yupo anakula maisha.

Kwa mujibu wa Mo J, mwanawe huyo analelewa katika mazingira mabovu yasiyokuwa na maadili na baba wa kambo ambaye ni Crey.

Vita hiyo hiyo imefika pabaya ambapo Mo J ameapa kwenda na Polisi nyumbani kwa Gigy kumchukua mwanawe huyo huku ikidaiwa kama atafanya hivyo basi kuna mtu damu itamwagika.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii