Nai" Mastaa Acheni Pombe Kali na Bata Zisizokuwa na Maana Kwenu".

NAIRATH Ramadhan au Nai; ni video vixen na msanii wa Bongo Fleva ambaye kwa mara ya kwanza amefunguka sababu iliyomfanya apungue, kuwa ni pamoja na kupunguza matumizi mabaya ya pombe.

 mrembo huyo anasema kuwa, baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakimuuliza sana juu ya kupungua kwake, lakini ukweli ni kwamba sasa hivi anazingatia sana vyakula na mazoezi.

“Sababu ya kupungua kwangu ni kwamba nafanya sana mazoezi na siku hizi nimepunguza kula vyakula vya wanga na kutumia pombe kali.

“Hivyo kwa baadhi ya mastaa ambao wanataka kuwa kama mimi, jamani kwanza jifunzeni kupenda afya zenu, acheni kunywa pombe kali na bata zisizokuwa na maana yoyote ile kwenu, hii itawasaidia kupata muda mzuri wa kupumzika na kuweza kuamka mapema kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi,” anasema Nai ambaye bado ngoma yake ya Siyo Siazi Yao aliyomshikisha Sanja inaendelea kufanya vizuri.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii