Kwa muda mrefu wasanii wa muziki nchini Tanzania, Marioo na Mimi Mars wamedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini wakawa wanakanusha.
Lakini kama ujuavyo, penzi ni kikohozi kulificha huwezi hivyo nao wameshindwa kuendelea kuficha na sasa mambo ni mubashara.
Baada ya tukio la ugawaji wa tuzo za muziki wiki iliyopita ambapo Marioo alishinda tuzo mbili, wawili hao walikuwa pamoja wakisherekea na video zipo zikimuonesha Mimi Mars akiwa amelala na tuzo.
Hata hivyo, wikiendi iliyopita ndipo mambo yakawakolea, wakajikuta
wakijirekodi video na kusambaa mitandaoni wakiwa ufukweni asubuhiasubuhi
hivyo kama kuna aliyekuwa anabisha, basi aendelee kubisha.
Wote; Marioo na Mimi Mars ni wasanii wazuri, lakini tatizo nyota tu ambayo sasa wameamua kuisafisha.
Kwa mfano; inasemekana kwamba Marioo angekuwa na nyota kali, basi angeweza hata kuwa kwenye levo za akina Diamond Platnumz kwa kuwa ana kipaji kikubwa.
Baadhi ya wataalam wanasema kuwa na kipaji tu haitoshi bali msanii anahitaji kujibrand kwa kuongeza jitihada nyingine binafsi.