Msanii WizKid atunukiwa tuzo (plaque) ya Nyota wa Mchezo hii ni baada ya kuujaza ukumbi wa 02 Arena kwa siku tatu, ambapo ni Novemba 28, 29 na Disemba Mosi, ukumbi ambao unabeba watu takribani 20,000.
Tuzo hiyo (Plaque) ni kwaajili ya kutambua mchango na mafanikio ya msanii WizKid na kazi nzuri aliyoifanya hasa kuandika historia kubwa kwa kumaliza tiketi za show zake zote tatu 02 Arena, Jijini London Uingereza.
WizKid anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kutunukiwa tuzo hiyo (Plaque).