Vyama 8 vya Siasa Vyatishia Kujiondoa Azimio.

Vyama vinane vya kisiasa vimetishia kuondoka katika muungano mpya uliobuniwa karibuni wa Azimio la Umoja One Kenya ambao unaunga mkono urais wa kiongozi wa ODM Raila Odinga.
Katika taarifa ya Jumatano, Aprili 6, vyama vilivyojitambulisha kwa pamoja kama Mwanzo Mpya vilikashifu kutengwa wakati wa kufanya maamuzi muhimu katika muungano huo.
Wakiongozwa na gavana wa Machakos Alfred Mutua, kikao hicho kililalamika kuwa hawakufahamishwa kabla ya kuunganishwa kwa Azimio la Umoja na One Kenya Alliance, wakisema walijua hilo kupitia vyombo vya habari.
Kutokana na hali hiyo, Mutua alisikitika kwamba uongozi wa Azimio ulikuwa ukishirikisha vyama vitatu pekee: Jubilee, ODM na Wiper, na kuvifungia nje vingine vidogo vidogo.
“Hatujaonyeshwa stakabadhi za makubaliano ya Muungano na bado wanasisitiza tutie sahihi, hatutakubaliana na hilo, kuna jaribio la kuendesha zoezi la mchujo wa vyama kupitia makubaliano. Baadhi ya wagombea tayari wamejindaa kwa mchuano na kwa hivyo hamna kitu kama kufanya makubaliano," taarifa hiyo ilisema.
Vyama hivyo vidogo vilisema kwamba vimekuwa vikipuuzwa na vile vinavyohisi vina usemi zaidi katika muungano huo.
Kwa hivyo, vyama hivyo vilimtaka Raila kuwatambua kwa kuwajumuisha kwenye bodi ya uchaguzi na kuzingatia maoni yao kwani wanawakilisha kambi kubwa ya wapiga kura.
vyema vilivyotishia kujiondoa  katika muungano mpya uliobuniwa karibuni wa Azimio la Umoja  hivi hapa
1. Maendeleo Chap Chap- Alfred Mutua.
2. Muungano- Governor Kivutha Kibwana
3. Kenya Reform Party
4. Chama Cha Uzalendo
5. Democratic Action Party of Kenya (DAP-K)-Eugine Wamalwa
6. PPT 7. NARC- Charity Ngilu.
8. Maendeleo Democratic

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii