Wanajeshi wa Ufaransa waliotumwa Ukraine: Moscow inaona ni "ushiriki wa moja kwa moja" katika mzozo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ameelezea kutumwa kwa wanajeshi wa Ufaransa nchini Ukraine kwa ajili ya mafunzo na matengenezo ya vifaa—jambo lililofichuliwa Jumatatu na RFI—kama « ushiriki wa moja kwa moja » katika mzozo wa Ukraine.


Uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini Ukraine umeishangaza Moscow na kuamua kuzungumza. Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov, ametangazaleo Jumanne Novemba 17 kwamba Moscow imeionya Paris kuhusu uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini Ukraine, akitaja hatua hiyo kuwa ni ushiriki wa moja kwa moja katika mgogoro huo.

Amebainisha kuwa hali hiyo imepita hatua ya kutoa msaada kwa Ukraine na kugeuka kuwa vita ya moja kwa moja. "Sio wanajeshi wa Ufaransa tu, tunajua hilo. Tumeelezea wasiwasi wetu... Hili si tena kuhusu kuisaidia Ukraine, bali kuhusu ushiriki wa moja kwa moja katika vita," Sergey Lavrov amewaambia waandishi wa habari.

Siku ya Jumatatu, RFI ilifichua uwepo wa "Misheni Volia", kikosi kidogo cha wanajeshi wa Ufaransa nchini Ukraine kinachojihusisha na utunzaji wa vifaa vya kijeshi na utoaji mafunzo bila kushiriki moja kwa moja katika mapigano. Hatua hii ilikosolewa vikali na Urusi, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov, aliyeitaja kuwa ushiriki wa moja kwa moja kwenye mzozo huo. Hata hivyo, Ufaransa imetoa hususan idadi fulani ya zana za kisasa za kivita kwa Kiev: mizinga ya Caesar, ndege za kivita za Mirage 2000 na makombora yeye uwezo wa hali ya juu. Mkusanyiko wa zana mbalimbali ambao matengenezo yake yanahitaji utaalamu mkubwa

Kulingana na taarifa zetu, usaidizi huu wa kijeshi wa Ufaransa umekuwa ukichukua jukumu kubwa nchini tangu angalau majira ya joto ya mwaka 2026. Na kulingana na vyanzo vya habari vya RFI, ni muundo «mwepesi na unaoweza kubadilika», unaojumuisha «vikosi vidogo kwa ajili ya kazi ndogo." Wanatuambia kwamba ili kuficha uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa nchini Ukraine, misheni ya Gerfaut hutumika kama mstari wa mbele. Ni lango la kuingia Ukraine. RFI imeambiwa kwamba "wanajeshi wa Ufaransa waliotumwa Ukraine wanaombwa kusema kwamba wanaelekea Poland."

Misheni hii ya Gerfaut, iliyotambuliwa rasmi, ni kikosi cha kijeshi cha Ufaransa kilichopo Poland tangu mwezi Februari 2023 (hasa katika kambi ya Wedrzyn kaskazini magharibi mwa Poland) kama sehemu ya Misheni ya Usaidizi wa Kijeshi ya Umoja wa Ulaya nchini Ukraine (EUMAM-Ukraine), ambayo imeongezwa muda kwa miaka mingine miwili, hadi Novemba 15, 2028.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii