José María Neves amechaguliwa tena kuwa Rais wa Cape Verde

Rais wa Cape Verde, José María Neves, amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili kwa mujibu wa matokeo ya awali ya urais, akiwa na asilimia 63.8 ya kura zilizohesabiwa.

María Neves ameahidi kuendelea na juhudi za kuimarisha uhuru wa raia wa Cape Verde na kuhakikisha kwamba kuna umoja wa kitaifa na ukuwaji wa nchi hiyo.

Karibia wapiga kura 419,448 walishiriki uchaguzi mkuu Jumapili ya wiki iliopita Novemba 15.

José María, 66, alikuwa alitarajiwa kuibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambalo limeonekana kuwa thabiti katika masuala ya kidemokrasia katika eneo hilo linalokabiliwa na mapinduzi ya kijeshi.

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa na tume ya uchaguzi nchini humo katika kipindi cha siku tangu au sita zijazo.

José María Neves alichaguliwa Rais wa Cape Verde kwa mara ya kwanza mwaka 2021, baada ya kuhudumu kama Meya na Waziri Mkuu na Rais wa chama cha PAICV kati ya mwaka wa 2001 hadi 2016.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali, ameshinda uchaguzi huo dhidi ya wagombea wengine watano akiwemo mgombea wake mkuu Wakili Joana Rosa Amado, 61, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuwania uchaguzi wa urais nchini Cape Verde.

Joana Rosa Amado, ni wa pili kwa asilimia 31.4 na tayari ametangaza kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii