Ukraine, Urusi na Marekani zakubaliana kuwa na mazungumzo Novemba: Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema nchi yake, Urusi na Marekani zimekubaliana kuwa na mazungumzo ya pande tatu mwezi Novemba mwaka huu.

Licha ya kauli yake, Zelensky ameeleza kuwa hawajaamua ni wapi mkutano huo utafanyika.

Katika mahojiano na shirika moja la Habari la nchini Ukraine, Rais Zekensky alidai kuwa amepokea uthibitisho kutoka kwa Urusi kupitia Marekani kuwa Rais Vladimir Putin atahudhuria mazungumzo hayo.

“Tumekubaliana na Wamarekani wamethibitisha kuwa Putin amewaambia kwamba timu zetu zitakutana mwezi Novemba kwa mazungumzo kati ya Marekani, Urusi na Ukraine.” Amesema Rais Zelenskyy.

Abu Dhabi ni mojawapo na maeneo ambayo huenda mkutano huo ukafanyika lakini pia imeripotiwa kuwa inawezekana ukafanyika barani Ulaya.

Zelenskyy aidha amesema ni muhimu sana kwa bara Ulaya kuhusishwa kwenye mkutano huo.

Rais Zelenskyy pia amedai kwamba mazungumzo kuhusu usitishaji mashambulio dhidi ya miundombinu ya nishati au dhidi ya meli za mizigo, yanaweza kuwa sehemu ya agenda kwenye mkutano huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii