Rais Donald Trump amesema hajutii kuanzisha vita nchini Iran licha ya kwamba vita hivyo vitakuwa na athari kwa uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa nchini Marekani mwezi Novemba.
Wakati wa mahojiano na shirika la Habari la Fox, Trump ametupilia mbali ripoti kuwa wafuasi wake wana hasira kuhusu vita vya Iran, akisisitiza kwamba vita hivyo vitamalizika baada ya uchaguzi wak Wabunge nchini Marekani.
Trump aidha amedai kuwa iwapo angehitajika kuishambulia tena Iran, angefanya hivyo bila kujutia hatua zake.
"Hapana, sidhani... yaani, siamini katika dhana ya kujutia. Unaweza kujiuliza maswali kidogo tu, na baadhi ya watu wameniuliza hivyo. Kama ningepata fursa ya kufanya hivyo tena, ningefanya vile nilivyofanya. Niliondoa uwezo wao wa nyuklia." Amesema Rais Trump
Marekani na Israel ziliishambulia Iran tarehe 28 ya mwezi Ferbuari, hatua ambayo ilipelekea Iran kujibu mashambulio hayo kwa kulenga kambi za jeshi la Marekani Mashariki ya kati.
Trump amekuwa akisema kwamba lengo la kuanzisha vita nchini Iran ni kupunguza na kuhoofisha uwezo wa Iran kuwa na silaha za nyukilia.