Uingereza na Ufaransa zimeafikiana kuhusu mkataba mpya wa miaka mitatu unaolenga kukomesha uhamiaji haramu kwa njia ya mkondo wa bahari uunaopita kati ya mataifa hayo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na pande zote, Ufaransa imeahidi kuongeza maafisa wa kuwadhibiti wahamiaji kwa zaidi ya asilimia 50, hadi kufikia maafisa 1,400 ifikapo mwaka 2029 pia itatumia teknolojia zaidi za ufuatiliaji kama droni na helikopta.
Nayo Uingereza itatoa zaidi ya dola
milioni 800, huku takribani robo ya fedha hizo zikitegemea mafanikio ya
kuwadhibiti wahamiaji yatakayokaguliwa kwa pamoja kila mwaka.
Mkataba huo unatokana na miezi kadhaa ya mazungumzo, ambapo London ilisisitiza masharti magumu zaidi baada ya kuishutumu Ufaransa kwa kutoweka juhudi za kutosha kuwazuia wahamiaji wasio na vibali.
Tangazo hilo limetolewa wakati Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, akikabiliwa na shinikizo la kisiasa la kudhibiti uhamiaji.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime