Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaweka utaratibu wa kugharamia matibabu kwa majeruhi wa ghasia za Oktoba 29, mwaka huu ambao bado wanahitaji msaada wa matibabu.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 alipohutubia wakati wa hafla ya makabidhiano ya ripoti ya tume ya uchunguzi wa ghasia za wakati na baada ya uchaguzi. “Serikali itaweka utaratibu wa kugharamia matibabu kwa majeruhi wa ghasia za Oktoba 2025 watakaothibitika na ambao bado wanahitaji msaada wa matibabu,” amesema.
Amesema Serikali pia itagharamia vifaa saidizi na viungo bandia kwa waliopata ulemavu wa kudumu kwenye ghasi hizo ili waweze kuyamudu mazingira yao ya kila siku.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime