Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa watatoa kiasi cha euro milioni 275 kama msaada wa kiutu kwa ajili ya watu wanaoishi katika maeneo yenye migogoro Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.
Mataifa yaliyotajwa kuwa yatapokea msaada huo ni yale yanayokabiliwa na mizozo, ukosefu mkubwa wa chakula na wimbi kubwa la wakimbizi Chad itapokea sehemu kubwa zaidi ya mgao huo, ikiwa na zaidi ya euro milioni 72. Euro milioni 75 zimetengwa kushughulikia migogoro mikubwa ya njaa huko Sahel ya Kati.
Nigeria itapokea euro milioni 33,
kutokana na kile Ulaya ilichokitaja kuwa mgogoro mbaya zaidi wa chakula katika
miaka ya karibuni.
Nchi nyingine zitakazopokea fedha hizo ni Jamhuri ya Afrika ya Kati, Cameroon na Mauritania. Mataifa ya pwani ya Afrika Magharibi, yakiwemo Benin, Ivory Coast, Ghana na Togo, yatapokea pia sehemu ya msaada huo. Ulaya imesema msaada wake unaonesha dhamira yake ya kukabiliana na hali mbaya ya kiutu barani Afrika.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime