RAIS SAMIA ATANGAZA HATUA ZA SERIKALI KUHUSU MATUKIO YA OKTOBA 29

Rais wa Tanzania MHE.DKT Samia Suluhu Hassan ametangaza hatua kadhaa za serikali kufuatia matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, 2025, akisisitiza dhamira ya kuleta maridhiano na kuhakikisha haki inapatikana kwa wote walioathirika.

Akizungumza hii leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati wa upokeaji wa ripoti ya Tume ya Rais iliyochunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Rais Samia alisema serikali itaunda tume ya maridhiano itakayokusanya maoni ya wadau mbalimbali, alieleza kuwa mapendekezo ya tume hiyo yatasaidia kuelekeza mchakato wa kupata katiba mpya.

Aidha, ametangaza kuundwa kwa chombo maalumu kitakachochunguza kwa kina masuala ya jinai yaliyosababisha vurugu hizo. Chombo hicho kitakuwa na jukumu la kubaini wahusika wote, wakiwemo waliofadhili, waliotekeleza pamoja na walioratibu matukio hayo.


Katika hatua nyingine, chombo hicho pia kitapewa jukumu la kuchunguza kwa undani suala la miili ya watu ambao bado haijapatikana, kwa lengo la kubaini ukweli na kutoa majibu kwa familia zilizoathirika.

Vilevile, serikali imeahidi kugharamia matibabu ya waathirika wote wa matukio hayo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kutoa msaada na kurejesha hali ya kawaida ambapo hatua hizi zinaashiria azma ya serikali ya kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na utawala wa sheria nchini.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii