Tume: Askari 16 waliuawa Oktoba 29


Tume ya uchunguzi wa ghasia, wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, imebaini askari 16 wa vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama waliuawa katika matukio hayo ya mwaka jana.


Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande ameyasema hayo leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 alipozungumza wakati wa kukabidhi ripoti yake mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesema idadi hiyo ya vifo vya askari ni sawa na asilimia 3.1, huku askari 120 hadi Machi mwaka huu, walikuwa katika vituo vya kutolea huduma za afya wakipatiwa huduma.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii