Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni rahisi kuivunja amani, lakini si rahisi kuirejesha hivyo hatima ya Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania wenyewe ameeleza hayo leo Aprili 23,2026 wakati akipokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu Amani Oktoba 29, iliyotoa matokea yake leo Ikulu Dar es Salaam.
“Ni rahisi kuibomoa nchi, lakini ni vigumu kuijenga upya. Sote tufahamu kuwa hatima ya Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania wenyewe,” “
Nguvu ya ushawishi wa makundi ya nje yanavunja amani na kuibomoa nchi, lakini kurudisha amani, usalama na kuijenga nchi upya nchi yetu, ufanyika kwa msaada wenye masharti magumu ya kisiasa, kiuchumi na biashara, tuwe makini Watanzania ndio wajenga Tanzania,” ameongeza kuwa
“Tunapoibomoa hakuna mjombo wa kutusaidia, tutapata mikopo yenye masharti ya kiuchumi na kisiasa ili kuijenga upya, lakini wakati wa kuibomoa tunaweza kupata msaada kirahisi kabisa.”
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime