Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu Amani Oktoba 29, imesema ushahidi iliyokusanywa na tume hiyo imebaini miongoni mwa makundi yaliyoshiriki ghasia za Oktoba 29, yalikuwa na lengo la kuiba na kupora mali.
“Ushahidi wa moja kwa moja wa waathirika walioporwa mali zao au kuibiwa, pamoja na picha za kidijitali na mnato, mjongeo zinaonyesha namna ya vitendo vya wizi na uporaji uliofanywa na makundi hayo,” imeeeleza na kuongeza kuwa:
“Kwa mfano wizi na uporaji uliotokea kwenye maduka na maeneo ya biashara katika mikoa iliyotembelewa na Tume,”amefafanua mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Othman Chande.
Jaji Chande ameeleza hayo wakati akitoa taarifa ya matokeo ya ripoti ya tume hiyo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime
#RipotiYaTume #UkweliOkt29