Tume ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi, imesema jumla ya watu 518 walipoteza maisha kutokana na ghasia za siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
Kwa mujibu wa tume hiyo, mchanganuo wa vifo hivyo ulikuwa watu 182 Dar es Salaam, Mwanza (90), Mbeya (80), Arusha walipoteza maisha watu 53 na mikoa mingine watu 113.
Hayo yameelezwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande, alipozungumza wakati wa kukabidhi ripoti ya uchunguzi mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kati ya vifi hivyo, amesema 21 ni watoto ambao miongoni mwao 15 walikuwa na umri wa miaka 15 hadi 17, wanne walikuwa na miaka saba hadi 10 na wawili chini ya miaka mitano.
“Vifo 205 vilikuwa vya raia na 16 sawa na asilimia 3.1 vilikuwa vya maofisa na askari wa vyombo vya usalama,” amesema Jaji Chande.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime
#RipotiYaTume #UkweliOkt29