Tume ya uchunguzi wa ghasia wakati na baada ya uchaguzi, imesema hakuna ushahidi uliothibitisha kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la Kondo, jijini Dar es Salaam.
Hayo yameelezwa leo, Alhamisi Aprili 23, 2026 na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Othman Chande alipozungumza wakati wa halfa ya kukabiri ripoti yake mbele ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Kutokana na ushahidi na uchunguzi wa tume wa uwandani na kuzingatia hali ilivyoonekana katika makaburi hayo, pamoja na taarifa za wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi, tume imebaini kuwa madai ya kuwepo kwa makaburi ya halaiki katika eneo la kondo hayakuweza kuthibitika,” amesema.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime
#RipotiYaTume #UkweliOkt.29