Ongezeko la joto kali laathiri mifumo ya chakula duniani

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa kiwango kikubwa cha joto kinachoshuhudiwa duniani, kinaiweka mashakani mifumo ya upatikanaji wa chakula hali hiyo inahatarisha maisha ya zaidi ya watu bilioni 1 duniani.

Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), ongezeko la joto linalodumu kwa muda mrefu linasababisha uharibifu kwa mazao, mifugo, uvuvi na misitu.

Aidha ripoti hiyo iliyoaangazia pia hatari zinazoongezeka baharini, imesema wimbi la joto kali baharini liliathiri zaidi ya asilimia 90 ya bahari zote duniani mwaka uliopita, na kutishia akiba ya samaki.

Hata hivyo mkuu wa Ofisi ya shirika la Chakula ya Umoja wa Mataifa iliyo mjini Roma, Kaveh Zahedi ametoa wito wa kwa mataifa duniani kuchukua hatua za haraka ili kupunguza mabadiliko ya tabianchi, na kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema ili kuwasaidia wakulima na wavuvi kukabiliana na hali hiyo.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTim

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii