Ujerumani yawasilisha mkakati wa kijeshi kuimarisha ulinzi

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amewasilisha mkakati mpya wa Kijeshi wa Kitaifa wakati serikali yake ikijiandaa kukabiliana na "kitisho kikubwa cha usalama" wa nchi yake kutoka kwa Urusi.

Mkakati huo umewasilishwa huku Ujerumani ikirejesha mfumo wa watu kujiunga na jeshi kwa hiari ili  kuongeza idadi ya wanajeshi na kuliimarisha jeshi hasa baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Ingawa maelezo kamili kuhusu mkakati huo ni siri, Pistorius amesema mpango wake unajumuisha kulifanya jeshi la nchi hiyo, Bundeswehr kuwa lenye nguvu zaidi barani Ulaya.

Aidha muhtasari na mpango huo umejikita zaidi kwa Ujerumani kuwa na silaha za mashambulizi ya masafa marefu kwa usahihi mkubwa, mifumo thabiti ya ulinzi wa anga, na teknolojia za kisasa kama vile akili mnemba, na matumizi ya maroboti.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii