Papa Leo XIV amelitembelea gereza maarufu katika mji wa Bata, nchini Guinea ya Ikweta Ssiku ya leo Aprili 22,2026 ambapo ziara hiyo imekusudia kuangazia ukiukwaji wa haki za binaadamu ambao mashirika ya kimataifa yamekuwa yakiulaani.
Aidha kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani amelitembelea gereza hilo wakati Mashirika ya haki za binaadamu, yakiwemo Amnesty International, yakidai mfumo wa haki wa Guinea ya Ikweta unakabiliwa na ukamataji wa kiholela, mateso kwa wafungwa, na ukosefu wa uhuru wa mahakama.
Hata hivyo taifa hilo pia limekosolewa kwa kuwapokea wahamiaji waliorejeshwa kutoka Marekani katika makubaliano yenye utata ingawa kabla ya ziara hiyo, zaidi ya mashirika sabini ya haki za binaadamu yalimtaka Papa kutumia mamlaka yake ya kimaadili kulaani ukiukwaji wa haki hizo na kuwahimiza viongozi wa Afrika kulinda haki za wakimbizi na wafungwa.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime