Jakaya Kikwete ateuliwa mwakilishi maalum wa African Union

Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete, ameteuliwa kuwa Mwakilishi Maalumu wa African Union katika eneo la Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mjini Addis Ababa, uteuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya AU, Mahmoud Ali Youssouf.

Hata hivyo katika nafasi hiyo, Kikwete anatarajiwa kusaidia juhudi za kuimarisha amani, usalama na diplomasia ya kinga, pamoja na kushughulikia changamoto za kisiasa na migogoro katika ukanda wa Pembe ya Afrika.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii