Makaburi zaidi ya 3,000 yahamishwa Bukoba kupisha mradi wa machinga

Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera imekamilisha zoezi la kuhamisha makaburi zaidi ya 3,000 kutoka eneo la Kishenge kwenda Kata ya Buhembe, ikiwa ni maandalizi ya kupisha ujenzi wa jengo la kitega uchumi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga.

Zoezi hilo ni sehemu ya jitihada za manispaa katika kuboresha miundombinu ya mji na kuhakikisha matumizi bora ya ardhi, sambamba na kutoa mazingira rafiki kwa ukuaji wa sekta ya biashara ndogondogo.

Akizungumza kuhusu zoezi hilo, Afisa Mazingira wa Manispaa ya Bukoba, ndugu Joseph Tambuko, amesema kuwa makaburi zaidi ya elfu tatu yamehamishwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja kwa kufuata taratibu zote zinazohitajika.

Aidha, Tambuko amebainisha kuwa miili 67 ilizikwa katika makaburi ya mtu mmoja mmoja, ikiwa ni utekelezaji wa mahitaji maalum na kutoa heshima stahiki kwa marehemu pamoja na familia zao.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii