Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limeeleza chanzo cha kufungiwa kwa nyota wa timu ya taifa, Jackline Sakilu, kwa miaka 10 kutokana na ukiukaji wa sheria za michezo.
Athari hiyo imetolewa na Athletics Integrity Unit (AIU) baada ya mwanariadha huyo wa mbio ndefu za barabarani (marathoni) kubainika kutumia dawa zilizopigwa marufuku.
Taarifa ya AIU imebainisha kwamba adhabu hiyo ilianza rasmi Septemba 17, 2025 na itadumu hadi mwaka 2035, hivyo kumfanya Sakilu kushindwa kushiriki mashindano yote ya kimataifa.
Uchunguzi umeonyesha kuwa mwanariadha huyo alikuwa na viambato vinavyohusiana na homoni ya testosterone, ambavyo vinapigwa marufuku katika riadha.
Hatua hii inahitimisha masuala yote ya kisheria na kimsingi inalenga kudumisha uadilifu katika michezo ya riadha.
10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime