Iran "Mapendekezo yaliowasilishwa na Marekani yanapitiwa na mamlaka"

Katika mahojiano na televisheni ya kitaifa, Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Abbas Araqchi, aliweka wazi kuwa mapendekezo ya Marekani ya kumaliza vita yanapitiwa na mamlaka ya juu jijini Tehran.

Licha ya kuthibitisha kwamba nchi yake inapitia mapendekezo ya Marekani, alisistiza kuwa ujumbe wanaoupokea kupitia kwa wapatanishi hauwezi kuchukuliwa kama mazungumzo.

Matamshi yake Araqchi yalionyesha nia ya Tehran kufanya mazungumzo ya kumaliza mapigano iwapo marsharti yake yatazingatiwa.

Alisisitizia msimamo wa Tehran kwamba ujumbe wanaopata kutoka kwa Marekani kupitia kwa wapatanishi sio mazungumzo kama inavyodaiwa na Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Israeli Channel 12, mpango wa Rais Trump uliowasilishwa hwa Iran kupitia kwa Pakistani unajumuisha, Shuguli katika vinu vya nyukilia vya Natanz, Fordow na Isfahan zitasitishwa na vinu hivyo kuharibiwa.

Shirika la nishati ya Atomiki (IAEA) litapewa nafasi ya kufuatilia kwa uwazi shughuli zinazohusiana na nyukilia nchini Iran miongoni mwa mengine.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii