Bei ya Mafuta Yapanda Tanzania Kufuatia Mzozo wa Mashariki ya Kati

SERIKALI ya Tanzania imetangaza kupanda kwa bei ya mafuta kuanzia Aprili 1, 2026, kufuatia athari za mzozo wa kivita katika eneo la Mashariki ya Kati unaohusisha Marekani, Israel na Iran.

Kupanda huko kumechangiwa na mashambulizi katika miundombinu ya mafuta pamoja na kufungwa kwa Lango la Hormuz, njia muhimu inayopitisha takribani asilimia 20 ya mafuta duniani.

Kwa mujibu wa EWURA, ongezeko la gharama za uagizaji wa mafuta limepelekea bei mpya kupanda katika mikoa mbalimbali, ambapo Dar es Salaam petroli ni Sh. 3,820, dizeli Sh. 3,806 na mafuta ya taa Sh. 3,684, huku baadhi ya maeneo yakifikia zaidi ya Sh. 4,000 kwa petroli.

Aidha EWURA imewataka wafanyabiashara kuzingatia bei elekezi na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka.

Hata hivyo wananchi wametakiwa kutumia mafuta kwa uangalifu wakati serikali ikiendelea kufuatilia hali ya soko la dunia, huku ikisisitiza kuwa akiba ya mafuta iliyopo nchini inaweza kudumu kwa takribani miezi mitatu.

10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii