Mkuu wa wilaya aridhishwa na maendeeo ujenzi uwanja wa ndege Msalato ‘Ring Road’

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri, akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje (Outer Ring Roads) jijini Dodoma.‎

‎ Mkuu wa Wilaya amesema kasi na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa ujenzi huo ni kubwa, na aimepongeza wakala wa barabara nchini (TANROADS) kwa kasi na hatua kubwa ya utelekezaji akieleza kuwa miradi hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi na kuboresha miundombinu ya usafiri makao makuu ya nchi nchi.‎

‎“Nimeridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato pamoja na barabara ya mzunguko. Hii ni miradi mikubwa na ya kimkakati kwa maendeleo ya Dodoma na Taifa kwa ujumla,” amesema Shekimweri.‎

‎Aidha, Mkuu wa idara ya miradi ya maendeleo mkoa wa Dodoma (TANROADS) Mhandisi Colman Ramadhani amesema uwanja miundombinu ya uwanja Hadi sasa Iko asilimia 83 na upande wa majengo ni asilimia 67 na pia amesemaWakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati uliopangwa.‎

‎Nayo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya imeeleza kuwa itaendelea kufuatilia kwa karibu miradi hiyo ili kuhakikisha inatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika na kuleta tija kwa wananchi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii