Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekosoa matokeo ya mazungumzo ya siku mbili mjini Geneva kati ya wawakilishi wa Ukraine na Urusi huku akisema hayakufikia matarajio kamili.
Hivyo rais huyo alikuwa anataka mazungumzo hayo yawe ni miongoni mwa mambo mengine yanayoangazia uwezekano wa kufanyika kwa mkutano kati yake na Rais Vladimir Putin.
Putin amesema mazungumzo kama hayo yanaweza kufanyika ila mjini Moscow tu, jambo ambalo Zelenskiy amelipinga.
Zaidi ya hayo Zelenskiy anasema alikuwa ameyataka mazungumzo hayo ya Geneva yajikite katika kuangazia masuala ya kiutu kama ubadilishanaji wa wafungwa na raia.
Hata hivyo Marekani kupitia msemaji wa ikulu ya White House Karoline Leavitt kwa upande wake imesema kumekuwa na hatua muhimu zilizopigwa kwenye mazungumzo hayo, huku kukiwekwa ahadi za ushirikiano katika kupata makubaliano ya amani.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime