Takaichi aapishwa tena kama Waziri Mkuu wa Japan

Sanae Takaichi ameapishwa tena kama waziri mkuu wa Japan, siku kumi baada ya ushindi wake mkubwa na wa kihistoria katika uchaguzi nchini humo.

Takaichi ameahidi kuuinua uchumi na kuimarisha ulinzi wa Japan ili kuilinda mipaka na bahari yake jambo ambalo huenda likaharibu uhusiano zaidi na China.

Mnamo Novemba iliyopita, Takaichi aliighadhabisha China kwa kusema huenda Japan ikaingilia kati kijeshi iwapo China itaichukua Taiwan kwa nguvu.

Waziri mkuu huyo wa Japan mwenye umri wa miaka 64,alikuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa nchi hiyo mnamo Oktoba na alishinda thuluthi mbili ya kura za wingi kwa chama chake katika uchaguzi ulioitishwa mapema bungeni mnamo Februari 8.

Hata hivyo ameelaza kuwa ushindi huo mkubwa alioupata unaonesha kuwa raia wa Japan wanataka mabadiliko muhimu ya kisera.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii