Bayer Leverkusen yaisogelea 16 bora Ligi ya Vilabu Bingwa

Klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, Bayer Leverkusen imepiga hatua muhimu katika kutinga raundi ya mtoano ya 16 bora ya Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya.

Hii ni baada ya kuilaza Olympiacos ya Ugiriki 2-0 katika mechi ya mchujo kuwania kusonga mbele, mshambuliaji wao kutoka Jamhuri ya Czech Patrick Schick akiwa mfungaji wa mabao yote.

Schick aliyafunga mabao yote hayo kwa kipindi cha dakika nne tu kabla kugonga dakika sitini ya mchezo.

Kwengineko Atletico Madrid ya Uhispania ilizuiwa sare 3-3 na Club Brugge kisha Bodo/Glimt kutoka Norway ikawashangaza Intermilan kwa kuwafunga 3-1.

Hata hivyo Newcastle ya England iliibamiza Qarabag ya Azerbaijan 6-1. ingawa Mechi za mkondo wa pili za duru hiyo ya mchujo zitachezwa wiki ijayo.

#10YrsJembefm  #Familiamoja #AhsantekwaTime

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii