Mwanza. Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine, amehimiza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hususan miundombinu ya barabara, ili kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi katika kata mbalimbali za jiji hilo.
Meya Sima ametoa rai hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mwanza kilichokutana kuidhinisha na kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Amesema fedha zilizoidhinishwa zitawezesha kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akibainisha kuwa kipindi hiki kisicho na mvua ni fursa muhimu ya kuimarisha ujenzi na ukarabati wa barabara pamoja na miundombinu mingine.
Kwa upande wake, Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Jeremiah Lubeleja, akiwasilisha rasimu ya bajeti mbele ya baraza hilo, amesema halmashauri inatarajia kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya kiutawala na miradi ya maendeleo.
Hata hivyo Bajeti hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ili kuendana na kasi ya ukuaji wa jiji la Mwanza.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa moja kamili jioni ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Evance Mlyakado tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime