Kwa mara ya kwanza baada ya takriban miaka 30, Waislamu na Wakristo duniani wameshuhudia kuanza kwa misimu yao mikuu ya kiroho kwa wakati mmoja — Ramadhan na Kwaresma.
Waislamu milioni duniani wameanza kufunga kuanzia alfajiri hadi machweo, kuadhimisha mwanzo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, ambao ni wa ibada, tafakari na kutoa sadaka.
Nchini Saudi Arabia, Qatar, Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na baadhi ya nchi za Afrika, Ramadhan imeanza Jumatano baada ya kuandama kwa mwezi, huku mataifa mengine yakitarajiwa kuanza Alhamisi kutokana na tofauti za uangalizi wa mwezi.
Wakati huo huo, Wakristo wameshika kipindi cha siku 40 cha Kwaresma, cha maombi, toba na tafakari.
Sherehe na ibada hizi zinafanyika katika mazingira tofauti — baadhi ya maeneo yakiwa katika vita huku waumini wakitafuta amani na matumaini.
Mwaka huu, misimu hii miwili ya kidini inakutana katika ujumbe mmoja wa pamoja: kufunga, kuomba, na kutafakari.
Katika dunia yenye migogoro na changamoto nyingi, waumini wa dini hizi mbili wanatumia kipindi hiki kuombea amani, msamaha na matumaini mapya.
Sasa ili kupata undani wa taarifa hii tafadhali usikose kutufuatilie na Usikilize jembe Habari Kamili hapo saa kumi kamili alasiri ambapo msomaji wetu wa hii leo ni Gloria Kiwia tafadhali usipitwe na taarifa zetu Mahiri kabisa.
Lakini pia tembelea mitandao yetu ya kijamii ya Jembefmtz
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime