Serikali ya Kenya imeripoti kupokea seti yake ya kwanza ya Lenacapavir, sindano mpya ya kinga dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (HIV) inayotoa ulinzi kwa hadi miezi sita kwa kipimo kimoja kwa watu wasiokuwa na maambukizi.
Wizara ya Afya ya Kenya imethibitisha kuwa takribani dozi 21,000 za awali tayari zimewasili nchini humo, zikiwa zimefadhiliwa na Global Fund.
Aidha mpango wa usambazaji wa dawa hiyo unatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi katika kaunti 15 zikiwemo Nairobi, Mombasa, Kisumu, Nakuru, Kiambu, Kakamega, Busia, Kilifi, Machakos, Kajiado, Uasin Gishu, Migori, Homa Bay, Kisii na Siaya.
Hata hivyo hatua hii inatajwa kuwa mafanikio makubwa kwa Kenya katika kuimarisha mikakati ya kupunguza maambukizi mapya ya HIV, huku ikiendeleza upanuzi wa mbinu za kinga kwa wananchi walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa.
#10YrsJembefm #Familiamoja #AhsantekwaTime